Community Advocacy on Environmental and Social Justice

Monday, 16 July 2012

WIMBO WA MAPAMBANO: KENYA


NI YALE YALE MAMBO YA UKOLONI

Niiyale, niyaleyale,
Mambo ni yale yale,
Nii yale, ni yale yale,
Mambo ya ukoloni    X2

1) Mambo, ni yaleyale,
Watu wetu… wetu wauwawa
Kila… kila mahali,
Nayote…yote kwa makombo
Wanao….wanaotupiwa
Na wadha…..limu wanyonyaji
Walimo..nchini mwetu,
Ngoma…..ni ile ile

Wooooi….. woii( silence or sounds of pain for 6 seconds)
Woiiye mambo ni yale yale,
Mambo ya ukoloni
Niiyale, niyaleyale,
Mambo ni yale yale,
Nii yale, ni yale yale,
Mambo ya ukoloni  

2) Tuna…… tuna nunua kuni,
  Kutoka, misitu yetu
Tuna tiririkwa na jasho,
Katika…. Ardhi yetu,
Na faida…. Ni kwa wadhalimu
Walio… tukalia,
Mapato , ya jasho letu
Hadithi… ni ile ile

Repeat chorus Wooi......

3)Chakula… chetu wakenya,
Tunacho… tolea jasho,
Chauzwa.. kile kizuri,
Tuna, tupiwa mabaki,
Ambapo…ambapo ingekuwa,
Na tule…. Kile kinono,
Chakula… chetu wenyewe,
Tunacho, tolea jasho………….

Repeat chorus Wooi......

4) Wabeberu… waliuwa wakenya,
Kwa njia… ya kuwa zuia,
Kupinga…uongozi wao,
Uongozi… wao wa mabavu,
Nasasa, serikali ya leo,
Inawauwa wakenya,
Kwa njia zile zile….
Walioridhi kwa wabeberu………..

Repeat chorus Wooi......

5) Maa - fundisho…
Mafundisho… sho ya wazalendo
Yatwambia kwamba…..
Unganeni mikono,
Tumwondoe adui wetu!
Na tu si … mamie utajiri
Na haki.. zetu wenyewe,
Na tufurahie matunda,
Matunda.. ya jasho letu….

Repeat chorus Wooi......

6) Tuuu…tu..tu……….
Tuuu tuta……
Tutavunja vunja
Vunja vunja ,
Tuta…tukakata…
Tuta bonda bonda
Minyororo ya wadhalimu x 2

Na tu pamoja na nyinyi,
Tu pamoja na nyi ( Vijana)
  ,,             ,,           ( Wa mama)
,,             ,,            (wazee……)

Mashujaa wa  Kenya


No comments:

Post a Comment

Hi Eroo !! Whats your Views on this ?